Halloween party ideas 2015
Showing posts with label Tanzania. Show all posts

Serikali imekanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa HOMA YA ZIKA nchini


Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema  ugonjwa wa homa ya ZIKA bado haujathibitishwa kuingia nchini na kuwatoa hofu wananchi ya uwepo wa ugonjwa huo hapa nchini.

Waziri MWALIMU amesema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu - NIMR ulikuwa ni utafiti uliofanyika nchini kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya ili kujua ubora wa  kipimo hicho.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo jiji DSM, wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi na wakunga 400.

Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amelishukuru shirika la AMREF Health AFRIKA TANZANIA kwa kuandaa mafunzo kwa wataalamu wa afya.

Katika harambee hiyo jumla shilingi milioni 290 zimechangwa huku lengo likiwa ni kukusanya shilingi milioni 500 ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.

Serikali inakusudia kupeleka bungeni muswada ili kutunga sheria ya taifa ya wazee itakayotoa wajibu wa kisheria kwa watoto na familia nzima kuwalea wazee wao na pia kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kuwanyanyasa wazee kwa lengo la kupunguza ama kutokomeza kabisa kero na mateso yanayowapata wazee nchini. Kauli hiyo imetolewa na waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee, mhe.

 Ummy Mwalimu kwenye maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Mbarali mkoani Mbeya. Katika hatua nyingine waziri Ummy Mwalimu ametoa miezi mitatu kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wote kwenye maeneo yao na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bure ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi inayoelekeza wazee nchini kupewa matibabu bure. Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema hadi kufikia mwezi juni mwaka huu, zaidi ya asilimia 78 ya wazee waliotambuliwa mkoani Mbeya walikuwa tayari wamepewa vitambulisho kwa ajili ya kupatiwa bure. Mfuko wa taifa wa bima ya afya ni miongoni mwa taasisi zinazotoa huduma ya matibabu kwa wazee ambao pia unao wajibu wa kuhakikisha wazee wanapatiwa matibabu ya bure

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto UMMY MWALIM amesema serikali imeagiza chanjo kutoka shirika la kimataifa la kuhudumia watoto
Shirika  la kuhudumia watoto duniaani UNICEF
.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto UMMY MWALIM amesema serikali imeagiza chanjo kutoka shirika la kimataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kuongeza kuwa tayari HAZINA imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 6.4 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.



Waziri UMMY amewambia waandishi wa habari mjini DODOMA kuwa baadhi ya chanjo zinatarajiwa kuwasili baadaye mwezi huu na kusambazwa kwenye vituo vyote vya afya  nchini.
Waziri UMMY amesema kuwa sio maeneo yote yenye upungufu wa chanjo, hivyo amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kukusanya na kutoa takwimu za upungufu huo.

September 16,2016

TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara, hali inayodaiwa kudhoofisha
 
TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa wataalamu  wenye ujuzi wa kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara,  hali  inayodaiwa kudhoofisha utoaji wa vipimo mbalimbali kwa wagonjwa.

Taarifa hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa Wakaguzi  wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini  unaofanyika  mkoani SINGIDA.

Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakaguzi wa Maabara Nchini Dakta MARGARET  MHANDO amesema kuwa mpaka sasa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wizara ina wataalamu watatu wa aina hiyo ambao hawakidhi mahitaji katika hospitali zilizopo hapa nchini.

Dakta MHANDO amewataka Wakaguzi  wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini  kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa maabara zote zilizopo nchini ili kuhakikisha maabara hizo zinatoa huduma na vipimo sahihi kwa wagonjwa.

 September 15, 2016
LEONARD MANGA
 == =

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema kuwa Wizara yake itaanzisha mpango wa Taifa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema  kuwa Wizara yake itaanzisha mpango wa Taifa wa kupima Saratani ya Shingo ya Uzazi na Matiti kwa Wanawake wote nchini.

Waziri UMMY MWALIMU amesema kuwa mpango huo unalenga kupunguza wagonjwa wanaofikishwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Jijini DSM wakiwa katika hatua za mwisho.
       
Waziri huyo wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ametoa kauli hiyo mkoani DODOMA wakati wa mafunzo ya Usimamizi na Udadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi hapa nchini.


September 15, 2016
IDD MAALIM
 == =

Baadhi ya hospitali jijini DSM hazina baadhi ya chanjo hali iliyowafanya watumishi wa hospitali na wagonjwa kuiomba serikali kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo

Wakizungumza na TBC wamesema kukosekana kwa chanjo hizo ikiwemo ya pepopunda kunaweza kusababisha vifo na ulemavu usiotarajiwa hususan kwa wajawazito, watoto wachanga na majeruhi wa ajali.

Taarifa za kukosekana kwa baadhi ya chanjo katika hospitali mbalimbali jijini DSM zikiwemo zile zinazotumiwa na wajawazito zimeifanya TBC kutembelea baadhi ya hospitali jijini humo ikiwemo Hospitali ya MNAZI MMOJA ili kufahamu hali halisi.

JANETH SUDA ni Muuguzi wa Afya ya Jamii, Mama, Baba na Mtoto katika Hospitali ya MNAZI MMOJA ambaye amesema chanjo ya tetenasi au pepo punda haipo katika hospitali hiyo.

Daktari kiongozi Hospitali ya Rufaa ya Amana STANLEY BINAGI ameonesha wasiwasi wa madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ukosefu wa chanjo hizo muhimu kwa binadamu.

Kupata ufafanuzi wa jitihada zinazofanywa na serikali kukabiliana na upungufu wa chanjo mwandishi wa TBC EDWARD KONDELA amezungumza na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. NEEMA RUSIMABAYILA ambaye amesema serikali imeagiza baadhi ya chanjo ikiwemo ya tetenasi au pepo punda zinazotarajiwa kufika kuanzia tarehe 19 mwezi huu, ambazo zitaweza kutumika kwa muda wa miezi mitatu.

September 9, 2016
 EDWARD KONDELA

Wazee wamelalamikia kutojumuhishwa katika mipango endelevu ya kitaifa SDG na kushindwa kupata mikopo katika mabenki , bima na mifuko ya vikoba kutokana na kuonekana hawafai kiuchumi

Wakizungumza wakati wa semina ya kuwashirikisha wazee kwenye malengo ya millennia iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa kiuchumi na kijamii ESRF na HELPAGE baadhi ya wazee hao wamesema pamoja na kupewa pensheni lakini fedha hizo hazitoshi kuanzisha mradi wowote wa maendeleo na kuwafanya kuwa masikini.

Kwa upande wake Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto UMMY MWALIMU amesema serikali imeanza kuwaondolea changamoto zote wazee kwa kuwaongezea kipato kwa kuwapa pensheni wazee wote, huduma za afya bure na wanatarajia kuanzisha mfuko wa wazee

 September 1, 2016

Dodoma. Wanajeshi wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) wamechangia chupa 30 za damu katika kituo cha damu salama Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Jumla ya maofisa 60 waliofnya zoezi la usafi na kuchangia damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya jeshi hilo.
JWTZ KUCHANGIA DAMU

Kamanda mkuu wakanda ya kati Brigedia Jenerali Masumbuko Mademe alisema jana kuwa wameamua kusherehekea siku iyo kwa kuchangia damu baada ya kupata taarifa  kuwa mkoa waDodoma kuna upungufu wa damu.

Pamoja na kuwalinda wananchi na mali zao tumeguswa tatizo la uhaba wa damu salama Dodoma tumeona ni vema sisi kuonyesha mfano wa kuchangia damu salama
Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma. Dk Charles kilogwe aliwaomba wakazi wa mkoa huo na taasisi nyingine za serikali kiuga mfano huo ili kunusuru maisha ya watanzania wanaopteza maisha kwa kukosa
damu.

Alisema mahitaji ya damu salama mkoani hapa lit 200 na kwamba wamekuwa wakikusanya lita 150.

Mamlaka ya Hali ya Hewa na Wizara ya Afya wamekutana kujadiliana namna ya kukabiliana na mabadailiko ya tabia nchi.


Mamlaka ya Hali ya Hewa na Wizara ya Afya wamekutana kujadiliana namna ya kukabiliana na mabadailiko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kusaidia kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu, Malaria na homa ya matumbo ambayo yanatokana na mabadiliko hayo.
Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa kimataifa uliohusisha nchi zaidi ya SITA Jijini DSM Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa , Profesa SUZANA NCHIMBI amesema mkutano huo utasiadia kuweka wigo mpana wa kukabiliana na maradhi ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu kati ya  nchi moja na nyingine.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti wa Mamlaka hiyo LADISLAUS CHAN’GA  amesema mabadiliko ya tabia nchi ni suala mtambuka hivyo ipo haja ya kuangalia kwa kina changamoto zake.
Mkutano huo wa siku tatu umeshirikisha nchi za KENYA,UGANDA, MADAGASCAR,ETHIOPIA,MALAWI ,  MAREKANI na mwenyeji TANZANIA.


 August 10, 2016
MWASU SWARE

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali zote za rufaa nchini ngazi ya Mikoa, Kanda na Hospitali ya Taifa Muhimbili kutoa matibabu bure kwa wagonjwa wa fistula.
Aliyasema hayo mjini Tanga kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Bombo katika uzinduzi wa kambi ya matibabu ya wagonjwa wa fistula itakayodumu kwa kipindi cha wiki moja kuanzia juzi hadi Agosti 19, mwaka huu.
Alisema tatizo la fistula limekuwa likiongezeka kila siku na waathirika wengi ni akinamama wa vijijini na wale wa kipato cha chini ambao wanashindwa kupata huduma sahihi za afya ikiwemo kuchelewa kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa kujifungua.
Takribani akinamama 2,500 hadi 3,000 hupata tatizo la ugonjwa wa fistula kila mwaka japo idadi hii ni ndogo sana kuliko hali halisi ilivyo kwa kuwa wagonjwa wengi hunyanyapaliwa na familia zao na jamii kwa ujumla.
“Serikali ya Awamu ya Tano imejikita zaidi katika kuwahudumia wanyonge, kwa mamlaka niliyopewa natoa msamaha wa kulipia matibabu ya fistula ili kuwapunguzia mateso wanawake hawa. Kwa kuwa wenye tatizo la fistula ni wanawake wa kipato cha chini na wa vijijini, naziagiza hospitali zote za rufaa za mikoa na kanda kutoa matibabu ya fistula bure kwa wagonjwa watakaofika kutaka huduma hiyo,” alisema Ummy.
Alisema ili kuhakikisha huduma hiyo inatolewa, ameziagiza hospitali hizo kuandaa kambi za matibabu ya fistula angalau mara moja kila mwaka na apatiwe taarifa.
Aidha, ameeleza kuwa akinamama wengi wenye tatizo la fistula wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli za uchumi kama biashara ndogo ndogo kwa kuwa ugonjwa huu ni wa aibu ambao husababisha watu kunyanyapaliwa na jamii.
Pia alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tatizo la ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma za ujauzito na uzazi, mafunzo ya huduma za dharura za uzazi kwa watoa huduma za afya pamoja na usimamizi shirikishi, uimarishaji wa ubora wa huduma za ujauzito na uzazi, kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya ujauzito na uzazi, kuimarisha mifumo ya rufaa na kuhakikisha huduma za dharura za uzazi zinapatikana hasa maeneo ya vijijini na wataalamu waliobobea katika maeneo hayo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Asha Mahita alisema Hospitali ya Bombo ina changamoto ya kuwa na miundombinu chakavu, uhaba wa vifaa tiba na watumishi kiasi ambacho wanashindwa kutoa huduma ya kutibu akinamama wenye tatizo la fistula kwa kuwa hawana wataalamu waliobobea katika maeneo hayo.

SIKU mbili baada ya gazeti la HABARI LEO kuchapisha habari kuhusu ugonjwa wa homa ya ini (Hepatitis B), kuwa hatari kutokana na kutokuwa na tiba, Serikali imeeleza sababu zilizochangia ugonjwa huo kugeuka kuwa tishio.
Katika toleo la juzi, gazeti hili lilieleza kuwa ugonjwa wa homa ya ini ni hatari kwa vile, unaua idadi kubwa ya watu kimya kimya, ambapo kati ya watu 100, watu wanane wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa huo.

Ilielezwa pia kuwa maambukizi ya ugonjwa huo ni makubwa mara 10 zaidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa, huugundua wakati ugonjwa uko kwenye hatua za mwisho na hivyo kusababisha mgonjwa kupoteza maisha.

Hayo yalibainishwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Tumbo na Ini, Idara ya Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk John Rwegasha katika mahojiano maalumu na gazeti hili juzi.
Hata hivyo jana akizungumzia ugonjwa huo na hatua zinazochukuliwa na serikali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema ugonjwa huo umekuwa tishio kwa vile haujapewa kipaumbele cha kutosha.

Mwalimu alisema maambukizi ya ugonjwa huo kwa hapa nchini yanaongezeka na kwamba pamoja na kuongezeka huko nchi haikuwa na takwimu sahihi zinazoonesha ukubwa wa tatizo.

Alisema baada ya kuona ukubwa wake, hivi sasa wizara imeanza mchakato wa kufanya marejeo ya Sera ya Afya ya Mwaka 2007 ili kuingiza ugonjwa huo kwenye magonjwa ya vipaumbele.
“Ni kweli ugonjwa huu ni hatari na kasi ya maambukizi hivi sasa inaongezeka, ingawa hatuna takwimu sahihi tulizozifanya wenyewe kwa kuwa hatukuupa kipaumbele ugonjwa huu kwa siku za nyuma, ila sasa tumeona ukubwa wa tatizo na tumeanza kuchukua hatua,” alisema Ummy.
Waziri huyo alibainisha kuwa serikali ilitilia mkazo zaidi kwenye chanjo kwa watoa huduma walio kwenye sekta ya afya tena kwa wale wanaohusika zaidi au moja kwa moja na wagonjwa na kuongeza kuwa kutokana na ukubwa wa tatizo kuna haja sasa ya kuangalia upya sera ya afya.
Alisema baada ya kufanya mapito ya sera hiyo wataangalia jinsi ya kujikita zaidi kwenye kinga ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo, ambao idadi kubwa ya wananchi hawana uelewa wa ugonjwa huo na athari zake, hadi pale mgonjwa anapougua.
Juzi akizungumzia dalili za homa ya ini, kwa aina zote mbili yaani B na C, Dk Rwegasha alisema mtu mwenye ugonjwa huo ni vigumu kumtambua hadi pale vipimo vya damu vitakapofanywa na kwamba kwa hapa nchini, hakuna mazoea ya kupima ugonjwa huo, hadi pale dalili zinapokuwa zimeanza kuonekana kwenye mwili wa mtu.
Dalili za ugonjwa huo kwa mujibu wa Dk Rwegasha ni pamoja na homa, tumbo kuuma upande wa juu kulia, kichwa mafua, macho kuwa na njano na wakati mwingine hata mkojo kuwa njano na pia wakati mwingine mtu aliyeathirika na ugonjwa huo hana dalili.
Alisema ugonjwa huo ni hatari na wakati mwingine zaidi ya Ukimwi kwa sababu ni ugonjwa unaoua watu wengi kimya kimya, na mtu anapogundua kuwa ameathirika na tatizo hilo, huwa ni kwenye hatua za mwisho na hivyo mgonjwa hupoteza maisha.

1–7 August 2016
World Breastfeeding Week is celebrated every year from 1 to 7 August to encourage breastfeeding and improve theHEALTH of babies around the world.
It commemorates the Innocenti Declaration signed in August 1990 by government policymakers, WHO, UNICEF and other organizations to protect, promote and support breastfeeding.
Breastfeeding is the best way to provide infants with the nutrients they need. WHO recommends exclusive breastfeeding starting within one hour after birth until a baby is 6 months old. Nutritious complementary foods should then be added while continuing to breastfeed for up to 2 years or beyond.
This year, WHO is encouraging people to “Support mums to breastfeed anytime, anywhere,” as all ofSOCIETY has a role to play in making our communities more breastfeeding-friendly.

Investigations carried by the ‘Sunday News’ discovered that students use unsafe water for domestic purposes, including drinking, cooking, washing and worse of all, drinking the water fresh from the lake without boiling it first, while surrounding villages relieve themselves in the lake.
A cross-section of school teachers and students who were interviewed by this paper said the school is afflicted with myriads of challenges, including lack of electricity, shortage of teaching staff and classrooms which are in bad shape.
ABOUT 303 students from Kipili Secondary School located along the shores of Lake Tanganyika in Nkasi District, Rukwa Region, are in danger of contracting water borne diseases due to drinking unsafe and unclean water from the lake, since the school lacks proper water infrastructure.

They added that the school environment is inhospitable and unsociable to both teachers and their students. Vice-Head of the School, Mr Calisto Mapunda, admitted that students at the school fetch water directly from Lake Tanganyika and use it for domestic purposes and worse still they drink it without boiling.
“Despite such challenges, the school has no science teacher, which compels some of us to teach the subjects including biology, mathematics, physics and chemistry in Form One and Two because it is compulsory for them (students) to study all the nine subjects. The school has only nine teachers, all of them are teaching art subjects,” added Mr Mapunda. Expounding further, he said that class-rooms are in bad shape with rough floors, some of them have neither doors nor windows and the walls have developed huge cracks.
On his part, Mr Chaua Zawadi, a history and civic subject teacher at the school said that even the parents and people living in the school vicinity have abandoned the school, with the opinion that it is the government’s responsibility to run and manage it.
“The schools surroundings are infested with different species of snakes including cobra, such reptiles are a threat to the lives of the students, for instance, the boys’ dormitory has no doors …. Equally Lake Tanganyika is also infested with crocodiles which can easily attack students when they are either fetching water or swimming,” said Mr Zawadi.

Similar sentiments were echoed by several students, including Loveness Chaula, Manuel Kamanki, Hosana Kalikula and Joseph Kakunda, who added that it is very pit that they are forced to sleep on the floor in their dormitories due to shortage of beds.

Reposted 

According to a statement, this first-of-its-kind multi-country collaborative cassava breeding initiative in East and Southern Africa is part of a major activity of the new cassava varieties and clean seed to combat CBSD and CMD (5CP) project which is funded by the Bill & Melinda Gates Foundation.
The project is led by International Institute of Tropical Agriculture (IITA) working in collaboration with the national agricultural research systems of Kenya, Malawi, Mozambique, Tanzania and Zambia where the trials are being conducted.
Disease resistance trials

The project is in its final year of implementation.
Dr Edward Kanju, IITA cassava breeder and coordinator of the 5CP project, said that preliminary results of the trials have already shown that several of the new varieties are virtually unaffected by CBSD and CMD, even in locations where disease pressure is extremely high from infected fields surrounding the trials. "Although in many of the countries the varieties are undergoing their first year of trials, our initial results are already showing good promise.

We will further validate the performance of these varieties by comparing them to local ones that have been selected as checks," he explained. This landmark regional initiative is aimed at speeding-up the breeding of cassava varieties with dual resistance to CMD and CBSD in the five countries where the diseases are of great concern. Each of the countries selected five of its best varieties in terms of performance against CMD and CBSD and shared them for the inter-country trials.
The planting materials first underwent a rigorous clean-up exercise to ensure they are virus-free before being distributed as tissue culture plantlets. This is the first time that breeders in the five countries have freely shared their best varieties in a concerted effort to tackle the two deadly diseases.
Dr James Legg, IITA virologist, highlighted another objective of the 5CP Project, which is the establishment of pilot clean seed distribution system in Tanzania, which he is leading. "We are perfecting the cassava seed systems in Tanzania through a three-step approach: Virus indexing, then rapid multiplication at a research station and finally large-scale multiplication at a clean site in an area with low disease pressure."

Dr Legg said that they have established clean seed sites in Mtwopa (Mtwara), Mwele (Tanga), Hombolo (Dodoma) and Nkenge (Kagera) in Tanzania's cassava-growing heartland. He added that they are routinely monitored and carefully managed and that he was happy to report that there have been very low incidences of CMD and CBSD in these sites.
"Moreover, the sites are now being used by the Tanzania Root and Tuber Research Programme to produce quality planting material of new, popular and disease-resistant varieties such as Mkuranga 1, Chereko, Kipusa and Kizimbani, as well as some of the older favourites, such as Mkombozi, Kiroba and Mumba," added Dr Legg.

The virus cleaning was carried out by the Natural Resources Institute (NRI) and the Kenya Plant Health Inspectorate (KEPHIS).
The material was forwarded to Genetics Technologies International Limited (GTIL), a commercial tissue culture company, for mass multiplication. The plantlets were then certified virus-free by the Mikocheni Agricultural Research Institute (MARI) and IITA.
Another major development of the project is the establishment of rapid multiplication systems for mini-plants derived from virus-indexed tissue culture plantlets.

By using these rapid propagation techniques in screen houses, the team led by Dr Kiddo Mtunda, cassava researcher and Officer-in-Charge of the Sugarcane Research Institute (SRI) in Kibaha, Tanzania and her team have been able to produce thousands of cassava plants in a matter of months. T

he success of this project offers promise not just for cassava producers in the target countries, but more widely to cassava producers throughout Africa.



Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA),wakati kikiadhimisha Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani mwaka huu kilibaini kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watoto walio chini ya miaka 14, wanakabiliwa na magonjwa ya kinywa na meno.
Pia kiilibaini kuwa asilimia 80 ya watanzania wanakabiliwa na matatizo ya ugonjwa wa fizi.
Katika kukabiliana na hali hiyo, wadau mbalimbali wameanza kutoa elimu ya afya ya kinywa ikiwa ni pamoja na watengenezaji wa dawa ya meno ya whitedent wa namna ya kujikinga na magonjwa ya kinywa.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliozungumza na East Africa Radio wanasema kumekuwa na upuuziaji mkubwa katika usafishaji wa meno, ulimi na kinywa kwa ujumla hali inayochangia watu wengi kung'oa meno yao.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Sophia Mjema amesema kuanzia sasa manispaa ya Ilala itamfikisha mahakamani mtu yeyote atakayegundulika anatupa taka barabarani kiholela.
Mkuu wa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Sophia Mjema amesema kuanzia sasa manispaa ya Ilala itamfikisha mahakamani mtu yoyote atakayegundulika anatupa taka barabarani kiholela huku kukiwa na mapipa maalum ya kutupia taka katika barabara za Samora na Sokoine.


        Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati alipoongoza wafanyakazi wa manispaa ya Ilala pamoja na wananchi kuweka mapipa 51 ya kutupia taka za aina zote katika barabara hizo.
Katika hatua nyingine wakazi wa Kawe jijini Dar es Salaam wametakiwa kujenga tabia ya kujitokeza kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ili kuhakikisha kata ya Kawe inakuwa katika hali safi ya mazingira.

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema inatarajia kuanza kutoa huduma ya kupandikiza vifaa vya kuongeza usikivu kwa watoto na figo kwa wenye matatizo hayo kuanzia mwakani.
Hospitali hiyo imesema inatarajia kuanza kuwapeleka wataalamu nje ya nchi kuanzia Septemba, mwaka huu kwa ajili ya kusoma kwa muda wa miezi miwili hadi minne ili Januari huduma hiyo ianze kutolewa.
Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Mseru wakati akiwatunuku vyeti wafanyakazi bora 53, ambapo alisema, kuanzishwa kwa huduma hiyo kutapunguza watoto waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi.
“…jambo hili tunatarajia kupunguza na kuondoa kitendo cha kuwasafirisha wagonjwa nje ya nchi kwani tunatarajia kutoa huduma ya kupandikiza vifaa vya kusikia kwa watoto wadogo, pia tutaanza kupandikiza figo,” alisema Profesa Mseru.

Alisema mbali na kutoa huduma hiyo hospitali hiyo inatoa huduma ya kusafisha figo, magonjwa ya tumbo, kufanya upasuaji mbalimbali huku akibainisha hospitali hiyo inahitaji ukarabati kutokana na miundombinu yake kuchakaa.
Profesa Mseru alisema, kutokana na ukubwa wa hospitali hiyo wamekuwa wakipokea idadi kubwa ya wagonjwa, huku miundombinu yake ikiwa na changamoto nyingi hasa katika kipindi cha mvua, upatikanaji wa vifaa vya kufulia nguo za wagonjwa, kuteketeza taka ngumu na vifaa vingine.
“Aidha, tuna upungufu wa rasilimali fedha katika utoaji huduma au kuwapa motisha wafanyakazi wetu,” alisema.
Alisema kila mwezi hospitali hiyo inalazimika kulilipa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Sh milioni 200 hadi 220 huku Shirika la Dawasco wakililipa Sh milioni 100 kwa mwezi.
Akizungumzia ulipaji wa majengo, Prof Mseru alisema Manispaa inawadai Sh milioni 20 kwa mwezi.Katika kipindi cha miezi 6 iliyopita wastani wa pato la hospitali kwa mwezi ilikuwa sh bilioni 2.3 hadi sh bilioni 2.5; huku mahitaji kwa mwezi ya kawaida ikiwa sh bilioni 4.
Mbali na hilo, Prof Mseru alisema wanatarajia kukarabati vyumba vya upasuaji na kuongeza kutoka idadi ya vyumba 13 hadi kufikia vyumba 19 na kuhakikisha vyumba vinakuwa vikubwa, sanjari na kuongeza vitanda katika chumba cha wagonjwa wenye uhitaji wa uangalizi(ICU), kutoka vitanda 21 hadi kufikia vitanda 60.

Powered by Blogger.