Wakizungumza na TBC wamesema kukosekana kwa chanjo hizo
ikiwemo ya pepopunda kunaweza kusababisha vifo na ulemavu usiotarajiwa
hususan kwa wajawazito, watoto wachanga na majeruhi wa ajali.
Taarifa za kukosekana kwa baadhi ya chanjo katika hospitali mbalimbali jijini DSM zikiwemo zile zinazotumiwa na wajawazito zimeifanya TBC kutembelea baadhi ya hospitali jijini humo ikiwemo Hospitali ya MNAZI MMOJA ili kufahamu hali halisi.
JANETH SUDA ni Muuguzi wa Afya ya Jamii, Mama, Baba na Mtoto katika Hospitali ya MNAZI MMOJA ambaye amesema chanjo ya tetenasi au pepo punda haipo katika hospitali hiyo.
Daktari kiongozi Hospitali ya Rufaa ya Amana STANLEY BINAGI ameonesha wasiwasi wa madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ukosefu wa chanjo hizo muhimu kwa binadamu.
Kupata ufafanuzi wa jitihada zinazofanywa na serikali kukabiliana na upungufu wa chanjo mwandishi wa TBC EDWARD KONDELA amezungumza na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Dkt. NEEMA RUSIMABAYILA ambaye amesema serikali imeagiza baadhi ya chanjo ikiwemo ya tetenasi au pepo punda zinazotarajiwa kufika kuanzia tarehe 19 mwezi huu, ambazo zitaweza kutumika kwa muda wa miezi mitatu.
September 9, 2016
EDWARD KONDELA

Post a Comment