Halloween party ideas 2015

Katika harakati za kutoa huduma ya malezi na ushauri kwa wanafunzi , VOICES walifika katika katika kata ya makurumula ,mtaa wa sisi kwa sisi, nyumbani kwa familia ya bwana Mwidete   na kufanya mahojiano na mwanafunzi ambaye tayari anapatiwa huduma ya malezi na ushauri kutoka kwa VOICES.

MAHOJIANO YAO YALIKUWA KAMA IFUATAVYO
1.Kwanza kabisa mwanafunzi aitwae Zera, aliweza kueleezea changamoto anazokutana nazo katika swala zima la elimu yake na malezi kwa ujumla ya kielimu kutoka kwa wazazi  na walimu wake, baadhi ya changamoto hizo zilikuwa ni
1. uhaba wa vitabu vya kiada na ziada
2. swala zima la usafiri
3. mtaara wa elimu.
4. upungufu wa idadi ya walimu mashuleni.

pia aliweza kuelezea changamoto za jumla zinazo kabili kada ya elimu Tanzania .
ushauri wake kwa serikali na wadau wote wa elimu waweze kuangalia kwa jicho la tatu  namna ya utatuaji wa  changamoto hizo kwa kufanya yafuatayo
1.kuongeza vitabu vya kiada na ziada mashuleni
2.kuleta usafiri kwa wanafunzi
3.kubadilishwa kwa mataara wa elimu
4. kuongezwa kwa idadi ya walimu mashuleni

Baada ya mahojiano  hayo mmoja wa wafanyakazi wa VOICES  aliweza kuelezea naman gani wao kama VOICES wanaweza kutatua changamoto hizo na kuongeza ubora wa elimu kwa wanafunzi kufauru vizuri mitihani yao , pia kuhakikisha  wanfunzi kufikia malengo yao kwa kutoa huduma ya malezi na ushauri wa kitaalamu . ............ UNAWEZA  KUANGALIA video  hapa  chini za mahojiano hayo     



Post a Comment

Powered by Blogger.