Serikali imekanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa HOMA YA ZIKA nchini
Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema
ugonjwa wa homa ya ZIKA bado haujathibitishwa kuingia nchini na kuwatoa
hofu wananchi ya uwepo wa ugonjwa huo hapa nchini.
Waziri MWALIMU amesema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu - NIMR ulikuwa ni utafiti uliofanyika
nchini kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na
chikungunya ili kujua ubora wa kipimo hicho.
Post a Comment