MUHTASARI
Nini maana ya VGP
VGP ni kifupisho cha VOICES GUIDANCE AND COUNSELLING PROGRAME
ambayo ni huduma inayotolewa na voices kwa lengo la kuwahamasisha wanafunzi na
wazazi kuwa na mtazamo chanya juu ya elimu,kunyanyua,na kuboresha taaluma
zao(Wanafunzi) ili waweze kupata manufaa wakiwa mashuleni ,majumbani kwao na
katika maisha yao ya baadae.
VOICES GUIDANCE AND COUNSELLING PROGRAME ni huduma
maalumu ambayo inatolewa na VOICES kwa lengo la kuwahamasisha wazazi
na wanafunzi katika kunyanyua na kuboresha taaluma ya mwanafunzi.
VOICES wanashrikiana na walimu wazazi, wanafunzi,watendaji
wa serekali hasa katika idara ya elimu (maafsa wa elimu wa halmashauri
mbalimbali) kwa lengo la kuhakikisha wazazi na hasa wanafunzi wanafikia malengo
yao kwa kuwapa ushauri mbali mbali na
kuwaonyesha kipasacho kufanya ili kufikia malengo.
Huduma hii kwa sasa inatolewa kwa GHALAMA NAFUU kabisa.
Walengwa wakuu wa kupatiwa huduma hii ni
i.
1. Wanafunzi wote waliopo ndani ya mkoa wa
dar es salaam (kwa sasa)
ii. 2. Wanafunzi wote waliopo dar es salaam
kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.
MAELEZO
KUHUSU HUDUMA
Huduma ya kuwasimamia wanafunzi katika maendeleo ya
shule hasa katika taaluma inatolewa na VOICES kwa kutengeneza muungano wa pamoja
kati ya VOICES, Wanafunzi, Wazazi/ Walezi,
pamoja na walimu.
VOICES watamsimamia mwanafunzi kuanzia ngazi aliyoko
mpaka mwanafunzi huyo aweze kutimiza malengo yake.
Makubaliano ya kumsimamia mwanafunzi huyu yatafanywa
kati ya VOICES pamoja na Mzazi au Mlezi na kuweza kuwashirikisha Walimu wa
shule asomayo mwanafunzi. Pia VOICES wataweza kushirikisha uongozi wa serikali
za mitaa waishio wanafunzi hao. Voices wanatarajia kutatua changamoto za
wanafunzi kama
i. 1.
Utoro mashuleni
ii. 2.
Ufaulu mdogo wa masomo
iii. 3.
Kutatua changamoto za kisaikolojia
zinazomkabili mwanafunzi
iv.
4.Ubunifu na njia bora za usomaji kwa
mwanafunzi
v. 5.
Kumwezesha mwanafunzi kutambua na
kuelewa malengo yake ya baadae
vi. 6.
Ukosefu wa elimu ya maisha nje ya shule
kwa wanafunzi
vii. 7.
Kupunguza mzigo kwa mzazi/mlezi juu ya
elimu ya mtoto
WALENGWA
WA HUDUMA
Walengwa Zaidi wa huduma hii ni wanafunzi
wote.VOICES watawasimia wanafunzi wa shule za msingi, Shule za Sekondary
(o-level and Advanced level) za kutwa na bweni.
Pia Voices watatoa huduma kwa wanafunzi waliomaliza
elimu yao Sekondari kwa kuwasaidia katika harakati za kutuma maombi katika vyuo
tofauti tofauti ili waweze kujiunga na elimu ya chuo kikuu na kuwafundisha mbinu
mbali mbali ambazo zitaweza kuwasaidia katika masomo yao ya baadae.
Pia kwa wanafunzi wa chuo na wa sekondari ambao
wanataka ajira za kudumu,voices ipo kwa ajiri yao.Tutawapatia maarifa ,mbinu na
ajira itakapobidi ili kuhakikisha wanafika lengo.
Voices haijawasahau wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa
kulipia ada ya shule za sekondari na chuo kikuu pamoja na mahitaji mengine ya
shule.
VOICES haitarajii mwanafunzi kufeli lakini ikitokea
kwa bahati mbaya mwanafunzi kafeli kwa
sababu ambazo labda zilikuwa nje ya uwezo wetu,VOICES watakuwa nae bega kwa
bega kwa kumtafutia njia mbadala ambayo itaweza kumsaidia katika maisha
yake,ikiwemo shughuli halali za uzalishaji mali.
MIKAKATI
i. 1.
Kufuatilia taarifa za wanafunzi
mashuleni.
ii.
2.Kupeleka taarifa hizo za wanafunzi kwa
wazazi wao na kuzitafsiri taarifa hizo kiupana Zaidi.
iii.
3.Kubaini changamoto zinazo mkabili
mwanafunzi mmoja mmoja.
iv.
4.Kutatua changamoto hizo kwa
Kuishirikisha idara ya elimu ya halmashauri husika (afisa elimu),
5.Kuwashirikisha Walimu, Wazazi , na uongozi wa serikali za mitaa.
v.
6.Kukagua madaftari ya wanafunzi,
kuhakikisha wanafunzi wanafanya majaribio na mazoezi (home work) pamoja na
mitihani.
vi.
7.Kuhakikisha wanafunzi hao wanafaulu
vizuri kazi hizo kwa ushirikiano uliopo kati ya mwalimu na VOICES.
vii.
VOICES watawaombea majaribio ya wiki
watoto wote ambao tutakuwa tumewasajiri kwa walimu wao wa masomo ili kuwafanya
watoto wawe wamebanwa na kazi za shule ili waweze kujisomea. Majaribio haya yatasimamiwa
na Mzazi mwenyewe na VOICES. Majaribio haya yatakusanywa na VOICES na
kumkabidhi mwalimu wa somo kusahihisha
lakini kwa idhini ya mwalimu VOICES wataweza kusahihisha majaribio hayo. Kisha
matokeo yao ya wiki yatarudishwa kwa mzazi pamoja na mwanafunzi,VOICES atakaa
pamoja na mzazi kujadili matokeo mwanafunzi ya jaribio husika.
VITENDO
NA UPIMAJI MATOKEO.
Mawakala wa VOICES watahitajika wafanye majukumu
yote watakayoelekezwa kikamilifu Zaidi na kuweza kuleta matokeo chanya. Upimaji
wa huduma utalenga kuangalia idadi ya wananchi wanao hitaji huduma na wameweza
kusaini form maalumu.
UTAWALA NA NGUVU KAZI
Timu ambayo inahusika kutekeleza shughuli ni ile
ambayo imepitishwa na Uongozi wa VOICES. Kwakuwa Utekelezaji wa shughuli hii
utachukua wanafunzi wengi ambao wanahitaji huduma. VOICES wataajiri watu wenye
sifa zifuatazo.
i. 1.
Awe amefaulu Mtihani wa kidato cha nne
au cha sita pamoja wahitimu wa chuo kwanzia astashada
ii.
2.Awe na moyo wa kujitolea.
iii.
3.Asiwe na historia ya uhalifu
KWA USAJIRI WA HUDUMA HII
Fika ofisini kwetu
Wilaya ya ubungo
KATA: Makurumla
MTAA: Sisi kwa sisi
Au wasiliana nasi kwa
Phone: 0685225275/0718403303/0713646855
Kwa maelezo Zaidi tembelea
http/www.voicestz.blogspot.com
IMEANDALIWA
NA UONGOZI WA VOICES TANZANIA
Post a Comment