Mganga Mkuu wa Serikali Profesa MUHAMMED KAMBI ametoa wito kwa
Wanasayansi nchini kujiridhisha katika tafiti zao na kutoa taarifa
ambazo zitakuwa na lugha rahisi inayoeleweka kwa jamii
.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa MUHAMMED KAMBI ametoa wito kwa
Wanasayansi nchini kujiridhisha katika tafiti zao na kutoa taarifa
ambazo zitakuwa na lugha rahisi inayoeleweka kwa jamii.
Profesa KAMBI ametoa wito huo Jijini DSM baada ya kushiriki
matembezi na uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa
yasiyoambukiza.
Profesa KAMBI pia amesisitiza kuwa kwa sasa hakuna Homa ya ZIKA
nchini na kuwataka wanasayansi nchini kufuata taratibu zilizopo wakati
wa kutangaza matokeo ya tafiti zao.
Mgeni rasmi katika matembezi na uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya
kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza alikuwa ni Makamu wa Rais SAMIA SULUHU
HASSAN ambaye ametoa muda wa miezi Mitatu kwa halmashauri zote nchini
kurudisha serikalini maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu mbalimbali.
Makamu wa Rais pia amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote
nchini kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja
na kutangaza kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa ni siku ya
mazoezi.
Kwa uapande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ALHAJ ALI HASSAN
MWINYI ametoa wito kwa Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda
afya zao.
Post a Comment