Halloween party ideas 2015

Wazee wamelalamikia kutojumuhishwa katika mipango endelevu ya kitaifa SDG na kushindwa kupata mikopo katika mabenki , bima na mifuko ya vikoba kutokana na kuonekana hawafai kiuchumi

Wakizungumza wakati wa semina ya kuwashirikisha wazee kwenye malengo ya millennia iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa kiuchumi na kijamii ESRF na HELPAGE baadhi ya wazee hao wamesema pamoja na kupewa pensheni lakini fedha hizo hazitoshi kuanzisha mradi wowote wa maendeleo na kuwafanya kuwa masikini.

Kwa upande wake Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto UMMY MWALIMU amesema serikali imeanza kuwaondolea changamoto zote wazee kwa kuwaongezea kipato kwa kuwapa pensheni wazee wote, huduma za afya bure na wanatarajia kuanzisha mfuko wa wazee

 September 1, 2016

Post a Comment

Powered by Blogger.