Halloween party ideas 2015

Serikali inakusudia kupeleka bungeni muswada ili kutunga sheria ya taifa ya wazee itakayotoa wajibu wa kisheria kwa watoto na familia nzima kuwalea wazee wao na pia kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kuwanyanyasa wazee kwa lengo la kupunguza ama kutokomeza kabisa kero na mateso yanayowapata wazee nchini. Kauli hiyo imetolewa na waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee, mhe.

 Ummy Mwalimu kwenye maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Mbarali mkoani Mbeya. Katika hatua nyingine waziri Ummy Mwalimu ametoa miezi mitatu kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wote kwenye maeneo yao na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bure ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi inayoelekeza wazee nchini kupewa matibabu bure. Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema hadi kufikia mwezi juni mwaka huu, zaidi ya asilimia 78 ya wazee waliotambuliwa mkoani Mbeya walikuwa tayari wamepewa vitambulisho kwa ajili ya kupatiwa bure. Mfuko wa taifa wa bima ya afya ni miongoni mwa taasisi zinazotoa huduma ya matibabu kwa wazee ambao pia unao wajibu wa kuhakikisha wazee wanapatiwa matibabu ya bure

Post a Comment

Powered by Blogger.