Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Sophia Mjema
amesema kuanzia sasa manispaa ya Ilala itamfikisha mahakamani mtu yeyote
atakayegundulika anatupa taka barabarani kiholela.
Mkuu wa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Sophia Mjema amesema kuanzia
sasa manispaa ya Ilala itamfikisha mahakamani mtu yoyote atakayegundulika
anatupa taka barabarani kiholela huku kukiwa na mapipa maalum ya kutupia taka
katika barabara za Samora na Sokoine.Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati alipoongoza wafanyakazi wa manispaa ya Ilala pamoja na wananchi kuweka mapipa 51 ya kutupia taka za aina zote katika barabara hizo.
Katika hatua nyingine wakazi wa Kawe jijini Dar es Salaam wametakiwa kujenga tabia ya kujitokeza kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ili kuhakikisha kata ya Kawe inakuwa katika hali safi ya mazingira.
Post a Comment