Taarifa hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa Wakaguzi wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini unaofanyika mkoani SINGIDA.
Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakaguzi wa Maabara Nchini Dakta MARGARET MHANDO amesema kuwa mpaka sasa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wizara ina wataalamu watatu wa aina hiyo ambao hawakidhi mahitaji katika hospitali zilizopo hapa nchini.
Dakta MHANDO amewataka Wakaguzi wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa maabara zote zilizopo nchini ili kuhakikisha maabara hizo zinatoa huduma na vipimo sahihi kwa wagonjwa.
September 15, 2016
LEONARD MANGA
== =
Post a Comment