Halloween party ideas 2015

Mamlaka ya Hali ya Hewa na Wizara ya Afya wamekutana kujadiliana namna ya kukabiliana na mabadailiko ya tabia nchi.


Mamlaka ya Hali ya Hewa na Wizara ya Afya wamekutana kujadiliana namna ya kukabiliana na mabadailiko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kusaidia kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu, Malaria na homa ya matumbo ambayo yanatokana na mabadiliko hayo.
Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa kimataifa uliohusisha nchi zaidi ya SITA Jijini DSM Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa , Profesa SUZANA NCHIMBI amesema mkutano huo utasiadia kuweka wigo mpana wa kukabiliana na maradhi ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu kati ya  nchi moja na nyingine.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti wa Mamlaka hiyo LADISLAUS CHAN’GA  amesema mabadiliko ya tabia nchi ni suala mtambuka hivyo ipo haja ya kuangalia kwa kina changamoto zake.
Mkutano huo wa siku tatu umeshirikisha nchi za KENYA,UGANDA, MADAGASCAR,ETHIOPIA,MALAWI ,  MAREKANI na mwenyeji TANZANIA.


 August 10, 2016
MWASU SWARE

Post a Comment

Powered by Blogger.