Shirika la kuhudumia watoto duniaani UNICEF |
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto UMMY MWALIM amesema serikali imeagiza chanjo kutoka shirika la kimataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kuongeza kuwa tayari HAZINA imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 6.4 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.
Waziri UMMY amewambia waandishi wa habari mjini DODOMA kuwa baadhi ya chanjo zinatarajiwa kuwasili baadaye mwezi huu na kusambazwa kwenye vituo vyote vya afya nchini.
Waziri UMMY amesema kuwa sio maeneo yote yenye upungufu wa chanjo, hivyo amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kukusanya na kutoa takwimu za upungufu huo.
September 16,2016
Post a Comment