Halloween party ideas 2015

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya ziwa imeteketeza kwa moto bidhaa mbalimbali ambazo haziruhusiwi kutumia na binadamu vikiwemo vyakula na vipodozi, ambavyo vimekamatwa katika oparesheni kali katika manispaa ya Musoma mkoani Mara baada ya kuingizwa nchini bila kuzingatia utaratibu.

Akizungumza wakati bidhaa hizo zikitekezwa katika dampo la halmashauri ya manispaa ya Musoma eneo la Buhare, mkaguzi mwandamizi wa TFDA Bw Julius Panga, amesema bidhaa hizo ambazo zimeteketezwa zimo ambazo hazijasajiliwa hapa nchini, ambazo zinadaiwa kuingizwa kwa njia za panya kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari. Nao baadhi ya maafisa afya wa halmashauri ya manispaa ya Musoma, wakizungumza wakati zoezi la uteketezaji wa bidhaa hizo likiendelea, wamewaonya wafanyabiashara wanaoingizi dawa na vyakula ambavyo haviruhusiwi kutumiwa na binadam hapa nchini.

Serikali inakusudia kupeleka bungeni muswada ili kutunga sheria ya taifa ya wazee itakayotoa wajibu wa kisheria kwa watoto na familia nzima kuwalea wazee wao na pia kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kuwanyanyasa wazee kwa lengo la kupunguza ama kutokomeza kabisa kero na mateso yanayowapata wazee nchini. Kauli hiyo imetolewa na waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee, mhe.

 Ummy Mwalimu kwenye maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Mbarali mkoani Mbeya. Katika hatua nyingine waziri Ummy Mwalimu ametoa miezi mitatu kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wote kwenye maeneo yao na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bure ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi inayoelekeza wazee nchini kupewa matibabu bure. Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema hadi kufikia mwezi juni mwaka huu, zaidi ya asilimia 78 ya wazee waliotambuliwa mkoani Mbeya walikuwa tayari wamepewa vitambulisho kwa ajili ya kupatiwa bure. Mfuko wa taifa wa bima ya afya ni miongoni mwa taasisi zinazotoa huduma ya matibabu kwa wazee ambao pia unao wajibu wa kuhakikisha wazee wanapatiwa matibabu ya bure

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto UMMY MWALIM amesema serikali imeagiza chanjo kutoka shirika la kimataifa la kuhudumia watoto
Shirika  la kuhudumia watoto duniaani UNICEF
.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto UMMY MWALIM amesema serikali imeagiza chanjo kutoka shirika la kimataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kuongeza kuwa tayari HAZINA imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 6.4 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.



Waziri UMMY amewambia waandishi wa habari mjini DODOMA kuwa baadhi ya chanjo zinatarajiwa kuwasili baadaye mwezi huu na kusambazwa kwenye vituo vyote vya afya  nchini.
Waziri UMMY amesema kuwa sio maeneo yote yenye upungufu wa chanjo, hivyo amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kukusanya na kutoa takwimu za upungufu huo.

September 16,2016

TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara, hali inayodaiwa kudhoofisha
 
TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa wataalamu  wenye ujuzi wa kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara,  hali  inayodaiwa kudhoofisha utoaji wa vipimo mbalimbali kwa wagonjwa.

Taarifa hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa Wakaguzi  wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini  unaofanyika  mkoani SINGIDA.

Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakaguzi wa Maabara Nchini Dakta MARGARET  MHANDO amesema kuwa mpaka sasa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wizara ina wataalamu watatu wa aina hiyo ambao hawakidhi mahitaji katika hospitali zilizopo hapa nchini.

Dakta MHANDO amewataka Wakaguzi  wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini  kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa maabara zote zilizopo nchini ili kuhakikisha maabara hizo zinatoa huduma na vipimo sahihi kwa wagonjwa.

 September 15, 2016
LEONARD MANGA
 == =
Powered by Blogger.