Halloween party ideas 2015

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto UMMY MWALIM amesema serikali imeagiza chanjo kutoka shirika la kimataifa la kuhudumia watoto
Shirika  la kuhudumia watoto duniaani UNICEF
.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto UMMY MWALIM amesema serikali imeagiza chanjo kutoka shirika la kimataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kuongeza kuwa tayari HAZINA imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 6.4 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.



Waziri UMMY amewambia waandishi wa habari mjini DODOMA kuwa baadhi ya chanjo zinatarajiwa kuwasili baadaye mwezi huu na kusambazwa kwenye vituo vyote vya afya  nchini.
Waziri UMMY amesema kuwa sio maeneo yote yenye upungufu wa chanjo, hivyo amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kukusanya na kutoa takwimu za upungufu huo.

September 16,2016

TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara, hali inayodaiwa kudhoofisha
 
TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa wataalamu  wenye ujuzi wa kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara,  hali  inayodaiwa kudhoofisha utoaji wa vipimo mbalimbali kwa wagonjwa.

Taarifa hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa Wakaguzi  wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini  unaofanyika  mkoani SINGIDA.

Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakaguzi wa Maabara Nchini Dakta MARGARET  MHANDO amesema kuwa mpaka sasa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wizara ina wataalamu watatu wa aina hiyo ambao hawakidhi mahitaji katika hospitali zilizopo hapa nchini.

Dakta MHANDO amewataka Wakaguzi  wa Maabara Binafsi kutoka mikoa yote nchini  kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa maabara zote zilizopo nchini ili kuhakikisha maabara hizo zinatoa huduma na vipimo sahihi kwa wagonjwa.

 September 15, 2016
LEONARD MANGA
 == =

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema kuwa Wizara yake itaanzisha mpango wa Taifa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema  kuwa Wizara yake itaanzisha mpango wa Taifa wa kupima Saratani ya Shingo ya Uzazi na Matiti kwa Wanawake wote nchini.

Waziri UMMY MWALIMU amesema kuwa mpango huo unalenga kupunguza wagonjwa wanaofikishwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Jijini DSM wakiwa katika hatua za mwisho.
       
Waziri huyo wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ametoa kauli hiyo mkoani DODOMA wakati wa mafunzo ya Usimamizi na Udadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi hapa nchini.


September 15, 2016
IDD MAALIM
 == =
Powered by Blogger.