Halloween party ideas 2015

Voices team ilifanikiwa kufika mkoani Dodoma na kushirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka Dodoma (DUWASA) katika kukagua miundombinu ya maji na kufanya maraekebisho, ikiwa ni moja ya njia ya kutaua kero za wananchi wa Dodoma.

           CHEMBA IKIZIBULIWA BAADA YA KUZIBA KWA UCHAFU.


Wanakikundi wa Voices waliweza pia kutoa elimu kwa wafanyabiashara mbali mbali pamoja na wanfunzi ambao walikua pembezoni mwa miundo mbinu hiyo ambayo ilikua hatarishi kwa afya zao na hata usalama wao.

Watanzania Wazalendo wameamua kutatua changamoto ya mueda mrefu ya upatikanaji wa dawa hapa nchini baada ya kuamua kujenga Kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa za binadamu ambacho mitambo yake itasimikwa eneo la Zinga wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Kiwanda cha Zinga Pharmaceuticals LTD ambacho uzinduzi wa ujenzi huo unatarajiwa kufanywa leo Machi 30, 2017 na Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto Jinsia na Wazee, Mhe. Dkt. Ummy Mwalimu, kitatengeneza dawa zenye standard ya Europe na kitakuwa na uwezo wa kusambaza dawa hizo Afrika Mashariki na Kati. 


Mitambo itakayozalisha dawa hizo itatoka Ujerumani na tayari wataalam wake wameshaingia nchini kwa ajili ya kuanza kufanya kazi hiyo muhimu.

Pombe nchini Urusi 
Takriban watu 41 wamefariki katika mji wa Serbia wa Irkutsk baada ya kunywa sabuni ya kuogea, kulingana na mamlaka ya Urusi

Sabuni hiyo ilio majimaji ilitumika kama pombe kulingana na kamati ya uchaguzi nchini Urusi. Watu
wengine 16 wako katika hali mbaya.
Tayari watu wawili wanazuiliwa kufuatia kisa hicho huku polisi wakionda chupa za sabuni hyo katika maduka.
Wachunguzi wanasema onyo kwamba sabuni hiyo haikufaa kutumika kama kinywaji lilidharauliwa.
Bidhaa hiyo ilikuwa na methanol, kemikali inayotumika kuyeyusha barafu.

Serikali imekanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa HOMA YA ZIKA nchini


Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema  ugonjwa wa homa ya ZIKA bado haujathibitishwa kuingia nchini na kuwatoa hofu wananchi ya uwepo wa ugonjwa huo hapa nchini.

Waziri MWALIMU amesema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu - NIMR ulikuwa ni utafiti uliofanyika nchini kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya ili kujua ubora wa  kipimo hicho.

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa MUHAMMED KAMBI ametoa wito kwa Wanasayansi nchini kujiridhisha katika tafiti zao na kutoa taarifa ambazo zitakuwa na lugha rahisi inayoeleweka kwa jamii
.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa MUHAMMED KAMBI ametoa wito kwa Wanasayansi nchini kujiridhisha katika tafiti zao na kutoa taarifa ambazo zitakuwa na lugha rahisi inayoeleweka kwa jamii.

Profesa KAMBI  ametoa wito huo Jijini DSM baada ya kushiriki matembezi na uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza.

Profesa KAMBI pia amesisitiza kuwa kwa sasa hakuna Homa ya ZIKA nchini na kuwataka wanasayansi nchini kufuata taratibu zilizopo wakati wa kutangaza matokeo ya tafiti zao.

Mgeni rasmi katika matembezi na uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza alikuwa ni Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ambaye ametoa muda wa miezi Mitatu kwa halmashauri zote nchini kurudisha serikalini maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu mbalimbali.

Makamu wa Rais  pia amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote nchini kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja na kutangaza kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa ni siku ya mazoezi.

Kwa uapande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ALHAJ ALI HASSAN MWINYI ametoa wito kwa Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.
Powered by Blogger.