Halloween party ideas 2015

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya ziwa imeteketeza kwa moto bidhaa mbalimbali ambazo haziruhusiwi kutumia na binadamu vikiwemo vyakula na vipodozi, ambavyo vimekamatwa katika oparesheni kali katika manispaa ya Musoma mkoani Mara baada ya kuingizwa nchini bila kuzingatia utaratibu.

Akizungumza wakati bidhaa hizo zikitekezwa katika dampo la halmashauri ya manispaa ya Musoma eneo la Buhare, mkaguzi mwandamizi wa TFDA Bw Julius Panga, amesema bidhaa hizo ambazo zimeteketezwa zimo ambazo hazijasajiliwa hapa nchini, ambazo zinadaiwa kuingizwa kwa njia za panya kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari. Nao baadhi ya maafisa afya wa halmashauri ya manispaa ya Musoma, wakizungumza wakati zoezi la uteketezaji wa bidhaa hizo likiendelea, wamewaonya wafanyabiashara wanaoingizi dawa na vyakula ambavyo haviruhusiwi kutumiwa na binadam hapa nchini.

Serikali inakusudia kupeleka bungeni muswada ili kutunga sheria ya taifa ya wazee itakayotoa wajibu wa kisheria kwa watoto na familia nzima kuwalea wazee wao na pia kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kuwanyanyasa wazee kwa lengo la kupunguza ama kutokomeza kabisa kero na mateso yanayowapata wazee nchini. Kauli hiyo imetolewa na waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee, mhe.

 Ummy Mwalimu kwenye maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Mbarali mkoani Mbeya. Katika hatua nyingine waziri Ummy Mwalimu ametoa miezi mitatu kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wote kwenye maeneo yao na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bure ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi inayoelekeza wazee nchini kupewa matibabu bure. Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema hadi kufikia mwezi juni mwaka huu, zaidi ya asilimia 78 ya wazee waliotambuliwa mkoani Mbeya walikuwa tayari wamepewa vitambulisho kwa ajili ya kupatiwa bure. Mfuko wa taifa wa bima ya afya ni miongoni mwa taasisi zinazotoa huduma ya matibabu kwa wazee ambao pia unao wajibu wa kuhakikisha wazee wanapatiwa matibabu ya bure
Powered by Blogger.