Halloween party ideas 2015

Pombe nchini Urusi 
Takriban watu 41 wamefariki katika mji wa Serbia wa Irkutsk baada ya kunywa sabuni ya kuogea, kulingana na mamlaka ya Urusi

Sabuni hiyo ilio majimaji ilitumika kama pombe kulingana na kamati ya uchaguzi nchini Urusi. Watu
wengine 16 wako katika hali mbaya.
Tayari watu wawili wanazuiliwa kufuatia kisa hicho huku polisi wakionda chupa za sabuni hyo katika maduka.
Wachunguzi wanasema onyo kwamba sabuni hiyo haikufaa kutumika kama kinywaji lilidharauliwa.
Bidhaa hiyo ilikuwa na methanol, kemikali inayotumika kuyeyusha barafu.

Serikali imekanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa HOMA YA ZIKA nchini


Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema  ugonjwa wa homa ya ZIKA bado haujathibitishwa kuingia nchini na kuwatoa hofu wananchi ya uwepo wa ugonjwa huo hapa nchini.

Waziri MWALIMU amesema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu - NIMR ulikuwa ni utafiti uliofanyika nchini kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya ili kujua ubora wa  kipimo hicho.

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa MUHAMMED KAMBI ametoa wito kwa Wanasayansi nchini kujiridhisha katika tafiti zao na kutoa taarifa ambazo zitakuwa na lugha rahisi inayoeleweka kwa jamii
.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa MUHAMMED KAMBI ametoa wito kwa Wanasayansi nchini kujiridhisha katika tafiti zao na kutoa taarifa ambazo zitakuwa na lugha rahisi inayoeleweka kwa jamii.

Profesa KAMBI  ametoa wito huo Jijini DSM baada ya kushiriki matembezi na uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza.

Profesa KAMBI pia amesisitiza kuwa kwa sasa hakuna Homa ya ZIKA nchini na kuwataka wanasayansi nchini kufuata taratibu zilizopo wakati wa kutangaza matokeo ya tafiti zao.

Mgeni rasmi katika matembezi na uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza alikuwa ni Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ambaye ametoa muda wa miezi Mitatu kwa halmashauri zote nchini kurudisha serikalini maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu mbalimbali.

Makamu wa Rais  pia amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote nchini kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja na kutangaza kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa ni siku ya mazoezi.

Kwa uapande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ALHAJ ALI HASSAN MWINYI ametoa wito kwa Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.
Powered by Blogger.