Halloween party ideas 2015

Mnamo tarehe 28/09/2017 VOICES  walikutana na wadau wa vijana na sio wengine ni RESTLESS DEVELOPMENT pale kawe kisiwani katika jengo la REGENT PARK . kwenye ofisi za RESTLESS DEVELOPMENT chini ya uongozi wa mradi KIJANA WAJIBIKA .
Voices wakiwa pamoja na Restless development katika moja ya shughuli za kijamii,kotoka kulia ni Mr kenny(restless),Mr Nuruel(voices),Miss Eliza(restless),Mr kingwaba(voices),Miss Veronice(voices) na Mr Dismass(restless)


MAMBO YAFUATAYO YALIJADILIWA KWA PAMOJA
1.Swala zima la kijana na uwajibikaji
namna gani vijana wanaweza kutumia fursa wanazokutana nazo katika kujinasua kiuchumi nz taifa kwa ujumla.

2. Afya ya jamii
jinsi ya kulinda na kuifanya afya ya jamii kuzidi kuimarika

3.VOICES GUIDANCE AND COUNCLING PROGRAME
Ni huduma iliyoanzishwa na voices ya kuwapati malezi bora wanafunzi wote Tanzania wa shule za msingi na sekondari.

pia voices na restless development  walifikia hitimisho  juu ya kufanya kazi kwa pamoja  kwa maendeleo ya TANZANIA yetu .

MUHTASARI 
Nini maana ya VGP

VGP ni kifupisho cha VOICES GUIDANCE AND COUNSELLING PROGRAME ambayo ni huduma inayotolewa na voices kwa lengo la kuwahamasisha wanafunzi na wazazi kuwa na mtazamo chanya juu ya elimu,kunyanyua,na kuboresha taaluma zao(Wanafunzi) ili waweze kupata manufaa wakiwa mashuleni ,majumbani kwao na katika maisha yao ya baadae.
VOICES GUIDANCE AND COUNSELLING PROGRAME ni huduma maalumu ambayo inatolewa  na VOICES kwa lengo la kuwahamasisha wazazi na wanafunzi katika kunyanyua na kuboresha taaluma ya mwanafunzi.

VOICES wanashrikiana na walimu wazazi, wanafunzi,watendaji wa serekali hasa katika idara ya elimu (maafsa wa elimu wa halmashauri mbalimbali) kwa lengo la kuhakikisha wazazi na hasa wanafunzi wanafikia malengo yao kwa kuwapa ushauri mbali mbali  na kuwaonyesha kipasacho kufanya ili kufikia malengo.
Huduma hii kwa sasa inatolewa kwa GHALAMA NAFUU kabisa.
Walengwa wakuu wa kupatiwa huduma hii ni
        i.            1. Wanafunzi wote waliopo ndani ya mkoa wa dar es salaam (kwa sasa)
      ii.            2. Wanafunzi wote waliopo dar es salaam kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.
    iii.            3.Kwa wanafunzi wa mikoa ya morogoro,pwani na tanga pia huduma hii inapatikana.


MAELEZO KUHUSU HUDUMA
Huduma ya kuwasimamia wanafunzi katika maendeleo ya shule hasa katika taaluma inatolewa na VOICES  kwa kutengeneza muungano wa pamoja kati ya VOICES, Wanafunzi, Wazazi/ Walezi,  pamoja na walimu.

VOICES watamsimamia mwanafunzi kuanzia ngazi aliyoko mpaka mwanafunzi huyo aweze kutimiza malengo yake.

Makubaliano ya kumsimamia mwanafunzi huyu yatafanywa kati ya VOICES pamoja na Mzazi au Mlezi na kuweza kuwashirikisha Walimu wa shule asomayo mwanafunzi. Pia VOICES wataweza kushirikisha uongozi wa serikali za mitaa waishio wanafunzi hao. Voices wanatarajia kutatua changamoto za wanafunzi kama
        i.         1.   Utoro mashuleni
      ii.           2. Ufaulu mdogo wa masomo
    iii.           3. Kutatua changamoto za kisaikolojia zinazomkabili mwanafunzi
    iv.            4.Ubunifu na njia bora za usomaji kwa mwanafunzi
      v.          5.  Kumwezesha mwanafunzi kutambua na kuelewa malengo yake ya baadae
    vi.          6.  Ukosefu wa elimu ya maisha nje ya shule kwa wanafunzi
  vii.          7.  Kupunguza mzigo kwa mzazi/mlezi juu ya elimu ya mtoto

WALENGWA WA HUDUMA
Walengwa Zaidi wa huduma hii ni wanafunzi wote.VOICES watawasimia wanafunzi wa shule za msingi, Shule za Sekondary (o-level and Advanced level) za kutwa na bweni.
Pia Voices watatoa huduma kwa wanafunzi waliomaliza elimu yao Sekondari kwa kuwasaidia katika harakati za kutuma maombi katika vyuo tofauti tofauti ili waweze kujiunga na elimu ya chuo kikuu na kuwafundisha mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwasaidia katika masomo yao ya baadae.
Pia kwa wanafunzi wa chuo na wa sekondari ambao wanataka ajira za kudumu,voices ipo kwa ajiri yao.Tutawapatia maarifa ,mbinu na ajira itakapobidi ili kuhakikisha wanafika lengo.
Voices haijawasahau wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kulipia ada ya shule za sekondari na chuo kikuu pamoja na mahitaji mengine ya shule.
VOICES haitarajii mwanafunzi kufeli lakini ikitokea kwa bahati mbaya mwanafunzi kafeli  kwa sababu ambazo labda zilikuwa nje ya uwezo wetu,VOICES watakuwa nae bega kwa bega kwa kumtafutia njia mbadala ambayo itaweza kumsaidia katika maisha yake,ikiwemo shughuli halali za uzalishaji mali.

MIKAKATI
        i.         1.  Kufuatilia taarifa za wanafunzi mashuleni.
      ii.            2.Kupeleka taarifa hizo za wanafunzi kwa wazazi wao na kuzitafsiri taarifa hizo kiupana Zaidi.
    iii.            3.Kubaini changamoto zinazo mkabili mwanafunzi mmoja mmoja.
    iv.            4.Kutatua changamoto hizo kwa Kuishirikisha idara ya elimu ya halmashauri husika (afisa elimu), 5.Kuwashirikisha Walimu, Wazazi , na uongozi wa serikali za mitaa.
      v.            6.Kukagua madaftari ya wanafunzi, kuhakikisha wanafunzi wanafanya majaribio na mazoezi (home work) pamoja na mitihani.
    vi.            7.Kuhakikisha wanafunzi hao wanafaulu vizuri kazi hizo kwa ushirikiano uliopo kati ya mwalimu na VOICES.
  vii.            VOICES watawaombea majaribio ya wiki watoto wote ambao tutakuwa tumewasajiri kwa walimu wao wa masomo ili kuwafanya watoto wawe wamebanwa na kazi za shule ili waweze kujisomea. Majaribio haya yatasimamiwa na Mzazi mwenyewe na VOICES. Majaribio haya yatakusanywa na VOICES na kumkabidhi  mwalimu wa somo kusahihisha lakini kwa idhini ya mwalimu VOICES wataweza kusahihisha majaribio hayo. Kisha matokeo yao ya wiki yatarudishwa kwa mzazi pamoja na mwanafunzi,VOICES atakaa pamoja na mzazi kujadili matokeo mwanafunzi ya jaribio husika.

VITENDO NA UPIMAJI MATOKEO.
Mawakala wa VOICES watahitajika wafanye majukumu yote watakayoelekezwa kikamilifu Zaidi na kuweza kuleta matokeo chanya. Upimaji wa huduma utalenga kuangalia idadi ya wananchi wanao hitaji huduma na wameweza kusaini form maalumu.

 UTAWALA NA NGUVU KAZI
Timu ambayo inahusika kutekeleza shughuli ni ile ambayo imepitishwa na Uongozi wa VOICES. Kwakuwa Utekelezaji wa shughuli hii utachukua wanafunzi wengi ambao wanahitaji huduma. VOICES wataajiri watu wenye sifa zifuatazo.
        i.           1. Awe amefaulu Mtihani wa kidato cha nne au cha sita pamoja wahitimu wa chuo kwanzia astashada
      ii.            2.Awe na moyo wa kujitolea.
    iii.            3.Asiwe na historia ya uhalifu

KWA USAJIRI WA HUDUMA HII
Fika ofisini kwetu
Wilaya ya ubungo
KATA: Makurumla
MTAA: Sisi kwa sisi
Au wasiliana nasi kwa
Phone: 0685225275/0718403303/0713646855
Kwa maelezo Zaidi tembelea
http/www.voicestz.blogspot.com

IMEANDALIWA NA UONGOZI WA VOICES TANZANIA










Zoezi la utoaji chanjo si jambo geni masikioni kwa wengi japokkuwa walio wengi hawazifahamu aina za chanjo zitolewazo katika vituo vya afya na umuhimu wake. Voices iliweza kubaini kuwa kuna kinamama wengi ambao wanhudhuria vituo vya afya pengine kupata chanjo binafsi au kuwapeleka watoto kupata chanjo bila kujiua aina ya chanjo hizo wala umuhimu wake.

 KISANDUKU CHA KUTUNZIA CHANJO
MTOTO AKIPEWA CHANJO AINA YA ROTA NA MUHUDUMU KUTOKA VOICES
Katika makala ija tutakwenda kuanisha aina zote za chanjo pamoja na umuhimu wake. Usikose kuendelea kutembelea blog yeko pendwa kuendelea kupata elimu hii.

Voices team ilifanikiwa kufika mkoani Dodoma na kushirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka Dodoma (DUWASA) katika kukagua miundombinu ya maji na kufanya maraekebisho, ikiwa ni moja ya njia ya kutaua kero za wananchi wa Dodoma.

           CHEMBA IKIZIBULIWA BAADA YA KUZIBA KWA UCHAFU.


Wanakikundi wa Voices waliweza pia kutoa elimu kwa wafanyabiashara mbali mbali pamoja na wanfunzi ambao walikua pembezoni mwa miundo mbinu hiyo ambayo ilikua hatarishi kwa afya zao na hata usalama wao.
Powered by Blogger.