Watanzania Wazalendo wameamua kutatua changamoto ya mueda mrefu ya upatikanaji wa dawa hapa nchini baada ya kuamua kujenga Kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa za binadamu ambacho mitambo yake itasimikwa eneo la Zinga wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Kiwanda cha Zinga Pharmaceuticals LTD ambacho uzinduzi wa ujenzi huo unatarajiwa kufanywa leo Machi 30, 2017 na Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto Jinsia na Wazee, Mhe. Dkt. Ummy Mwalimu, kitatengeneza dawa zenye standard ya Europe na kitakuwa na uwezo wa kusambaza dawa hizo Afrika Mashariki na Kati. 


Mitambo itakayozalisha dawa hizo itatoka Ujerumani na tayari wataalam wake wameshaingia nchini kwa ajili ya kuanza kufanya kazi hiyo muhimu.