SEKTA ZA AFYA KUIMAIRISHWA NCHINI TANZANIA
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya.
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo jiji DSM, wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi na wakunga 400.
Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amelishukuru shirika la AMREF Health AFRIKA TANZANIA kwa kuandaa mafunzo kwa wataalamu wa afya.
Katika harambee hiyo jumla shilingi milioni 290 zimechangwa huku lengo likiwa ni kukusanya shilingi milioni 500 ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.